Wachezaji wa zamani Ronaldinho, Hernan Crespo, Cafu, Gianluca Zambrotta, Roberto Carlos na Francesco Totti ni miongoni mwa wanasoka waliojiunga na Diego Maradona katika mechi maalum ya hisani iliyofanyika Jijini Roma nchini Italia.
Mchezo huo wa kuungana kwa amani, ulioandaliwa na Papa Francis umefanyika kwenye dimba la Stadio Olimpico, umuhimu wake umejionyesha kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wa zamani waliojitokeza.
Nyota wa zamani wa Argentina Maradona alikuwa kivutio pamoja na raia wa Italia Toti huku pia mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldinho akionekana kuwa kivutia katika mchezo ambao Wachezaji 11 bora wa zamani wa A La Liga XI waliibuka na ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya 11 bora wa dunia.
Diego Maradona akishangilia goli la Francesco Totti
Diego Maradona akidhibitiwa na Juan Sebastian Veron
Diego Maradona akikumbatiana na Ronadinho
Diego Maradona akisalimiana na Papa Francis baada ya kuombwa kushiriki mechi hiyo
0 comments:
Post a Comment