Tyson Fury ameachia mikanda yake ya ubingwa wa uzito wa juu ya WBO na WBA, kutokana kuwepo katika kipindi cha matibabu ya msongo wa mawazo.
Muingereza huyo, 28, alikiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine ili kukabiliana na msongo wa mawazo na inaelekea huenda akapoteza leseni yake ya ngumi.
Fury hakupigana tangu ampige Wladimir Klitschko Novemba mwaka 2015 na alijiondoa mara mbili kushiriki mapambano ya kurudiana na Klitschko.
0 comments:
Post a Comment