Real Madrid imepoteza nafasi ya kuvunja rekodi ya kushinda michezo 17 mfululizo katika Ligi ya La Liga baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Villarreal.
Wenyeji Madrid walijikuta wakifungwa goli baada ya Sergio Ramos kuuzuia kwa mkono mpira na Bruno Soriano kufunga kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo baadaye Sergio Ramos alirekebisha makosa yake baada ya tu ya kuanza kipindi cha pili kwa kufunga kwa kichwa mpira wa kona.
Sergio Ramos akiwa ameupiga mpira kwa kichwa ambao ulienda kujaa wavuni
Cristiano Ronaldo alidhibitiwa vilivyo na kushindwa kutikisa nyavu
0 comments:
Post a Comment