Mwanzo mzuri wa Mario Balotelli akiwa na klabu ya Nice umeendelea baada ya mchezaji huyo kutundika magoli mawili wakati wakiizamisha Monaco kwa magoli 4-0 katika mchezo wa Ligi 1.
Mshambuliaji huyo raia wa Italia alifunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza tangu ahamie Ligi ya Ufaransa, na jana tena alifumania nyavu katika vipindi vyote viwili.
Magoli mengine ya Nice yalifungwa na Paul Baysse aliyefunga la kwanza, huku Alassane Plea akikamilisha la nne na kuifanya Nice kuchuma pointi 14 katika michezo sita.
Mario Balotelli akiachia shuti na kuandika goli
0 comments:
Post a Comment