Ujenzi wa daraja la Salender lipitalo baharini kuanza mwakani

Rais Dk John Magufuli amesema kuwa ujenzi wa daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo la Aga Khan kupitia baharini jijini Dar es Salaam unatarajia kuanza mwezi Juni mwakani.

4

Ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar baada ya kufanya mazungumzo ya muda mfupi na balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, na kuongeza kuwa ujenzi huo unaanza baada ya serikali kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa mkandarasi.

“Process ya kulijenga hili daraja la Salender, zinaendelea vizuri,kwasababu sasa hivi kampuni ya kikorea inayofanya desgning iko kwenye hatua za mwisho, na tenda zinatarajiwa kutangazwa mwezi wa 3 mwaka kesho, na tenda zile zitaenda haraka na mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza ukaanza kati ya mwezi wa 6 mwaka kesho, ujenzi wa lile daraja linalopita baharini,” alisema Dk Magufuli.
Daraja la Salender litakuwa na urefu wa kilometa 7 zikiwemo kilometa 1.4 zitakazopita baharini. Kukamiliza kwa ujenzi huo kutasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari katika jiji la Dar.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment