Ubaguzi wa rangi umeripotiwa kuibuka nchini Marekani katika jimbo la Michigan kilipo Chuo Kikuu cha Michigan mashariki mwa jimbo hilo.
Taarifa kutoka katika Chuo hicho zimeeleza kuwa kumekuwepo vitendo vya ubaguzi wa rangi chuoni hapo ambapo wanafunzi weusi wenye asili ya kiafrika wananyanyapaliwa na wanafunzi weupe wa Kimarekani.
Mnamo tarehe Septemba 20 mwaka huu wanafunzi wa vitivo mbalimbali Chuoni hapo walishangazwa na kitendo cha kukuta maandishi yanayoashiria ubaguzi yakiwa yamechorwa katika moja ya kuta ya bweni chuoni hapo.
Kuta iliyochorwa kupeleka ujumbe kwa wanafunzi weusi chuoni hapo.
Maandishi hayo yaliyosomeka “KKK”, “LEAVE NIGGERS” yakiwa yamechorwa na kukolezwa kwa rangi nyekundu, bluu na nyeupe. Yamehusishwa moja kwa moja na tukio moja la kihistoria la nchini Marekani ambapo ubaguzi ulikua umekithiri, na watu weupe waliunda genge maarufu mwaka 1866 la kuzuia harakati za kupigania uhuru wa mtu mweusi na vitendo vya ubaguzi nchini Marekani maarufu kama ‘KU KLUX KLAN – KKK’.
Rais wa Chuo hicho Bwana James Smith amelaani vikali vitendo hvyo vya kibaguzi na kusema si sehemu ya maadili na mafunzo wapewayo chuoni hapo.
Rais wa Chuo hich, Bwana James Smith.
“Chuo kwa kushirikiana na Uongozi wa wanafunzi tunalaani vikali vitendo vya ubaguzi wa rangi na unyanyapaa, nan i kinyume na maadili, mazingirabna sheria za hapa chuoni kwetu” amesema James Smith.
Wafanya usafi chuoni hapo wamesafisha ukuta huo ili kuondoa hali yoyote ya hofu inayoweza kuzuka chuoni hapo, aidha rais wa chuoo hicho Bw James Smith amesema polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
Wafanya usafi wakisafisha ukuta huo.
0 comments:
Post a Comment