Muigizaji Jim Carrey adaiwa fidia kwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa mpenzi wake

the-mask

Muigizaji maarufu katika mji wa Hollywood nchini Marekani Jim Carrey amedaiwa fidia kwa kosa la kuchukua dawa kwa jina la uongo, na kusababisha kifo cha aliyekuwa mpenzi wake Cathriona White.
Bi Cathriona White amefariki mwaka jana na chanzo cha kifo chake kimetajwa na moja ya hati kutoka katika mahakama ya mji huo kuwa ni kuzidisha matumizi ya dawa za tiba kupindukia {Drug overdose}
Bwana Mark Button mume wa sasa wa Bi Cathriona amemtuhumu muigizaji Jim Carrey  kutumia vibaya umaarufu wake na wadhifa wake ili kupata dawa za tiba kinyume na sheria na kisha kujaribu kuficha kuhusika kwake na tukio hilo.
 Marehemu Bi Cathriona White mwenye asili ya nchini Ireland amepoteza uhai wake akiwa na umri wa miaka 30 ambae alikutwa amekufa kwa kuzidisha dozi ya Ambien, Propranolol and Percocet,
Taarifa za madai ya fidia zilizotolewa na Mahakam kuu ya mjini Los Angeles imeeleza kuwa Jim (54) alichukua dawa kutoka katika kituo cha dawa kwa jina la uongo la “Arthur King” na kisha kujaribu kuficha kuhusika kwake katika tukio hilo.
Hadi sasa muigizaji Jim Carrey hajatoa maelezo yoyote kuhusu tuhuma hizo.
Jim Carrey ameigiza filamu za vichekesho maarufu duniani kama ‘The mask’, ‘The cable Guy’, ‘Liar Liar’, ‘Dumb and dumber’ na nyinginezo.

jim-carrey-kulia-akiwa-na-aliyekuwa-mpenzi-wake-marehemu-cathriona-white
Jim-Carrey  akiwa na aliyekuwa mpenzi wake marehemu Cathriona White
mark-button-kushoto-akiwa-na-mkewe-marehemu-bi-cathriona-white
Mark Button  akiwa na mkewe marehemu Bi Cathriona White
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment