THEO WALCOTT AONYESHA MAKALI YAKE NA KUIPA USHINDI ARSENAL


Theo Walcott ameonyesha makali yake kwa kufunga magoli mawili wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Basel katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Iliwachukua washika mitutu dakika sita kupata goli la kwanza kupitia Walcott akifunga kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Alexis Sanchez.

Wachezaji hao wawili wa Arsenal walishirikiana tena na kutoa fursa kwa Walcott kufunga goli la pili kwa shuti la chini.
                                            Theo Walcott akifunga goli lake la kwanza kwa kichwa 
                                      Theo Walcott akianguka chini baada ya kutupia goli la pili
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment