Gerard Pique ameisaidia Barcelona kuongoza kundi C baada ya kuifungia goli la ushindi katika kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach.
Timu hiyo ya Ujerumani ilipata goli la kuongoza dhidi ya Barcelona, katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Thorgon Hazard.
Barcelona ilirejesha uhai wake baada ya kusawazisha kupitia kwa Arda Turan na kisha baadaye Pique kufunga la pili.
Beki Gerard Pique akifunga goli la pili lililoipa ushindi Barcelona
0 comments:
Post a Comment