Watu wanne wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara, baada ya moja kati ya magari yaliyokuwa katika msafara wa Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hasssan Kupata ajali.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Nanguruwe takribani kilomita 45 kutoka Mtwara mjini.
Ajali hiyo imetokea wakati Makamu wa Rais alipokuwa njiani kuelekea wilayani Tandahimba kutembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu mkoani mtwara.
0 comments:
Post a Comment