MOTO WA NYIKA WASABABISHA MAELFU KUHAMISHWA HISPANIA


Maelfu wamehamishwa kutoka kwenye miji nchini Hispania ambayo pia imefurika watalii kufuatia moto mkubwa wa nyika eneo la Costa Blanca.

Picha zilizopigwa zinaonyesha moto mkubwa karibu na eneo la Xabia, kusini mwa Valencia huku kukiwa na hofu kuwa moto huo umewashwa kwa makusudi jana.

Watalii wa nje na ndani pamoja na wakazi wa miji iliyokumbwa na moto huo wamehamishiwa kwenye majengo ya shule na hoteli, huku nyumba 20 zikiwa zimeteketea kwa moto.
                                     Moto wa nyika ukiteketeza majengo katika Costa Blanca

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment