DARAJA REFU LA KIOO NCHINI CHINA LAFUNGWA BAADA YA KUFUNGULIWA KWA SIKU 13 TU


Daraja refu la kioo nchini China ambalo lilivunja rekodi wakati lilipofunguliwa limefungwa baada ya kutumika kwa siku 13 tu.

Maafisa wa China wanasema serikali inapanga kulifanyia matengenezo daraja hilo ambalo limefungwa jana Ijumaa, siku ya kufunguliwa tena itatangazwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa CNN, msimamizi wa daraja hilo la kioo amewaambia daraja hilo lilizidiwa na idadi ya watu wanaotembelea na kulitumia.
Watu wakikatiza juu ya daraja hilo mara baada ya kufunguliwa kabla ya kufungwa Ijumaa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment