CHARLIE AUSTIN ATUPIA MBILI WAKATI SOUTHAMPTON IKISHINDA



Charlie Austin amefunga magoli mawili wakati Southampton ikipata ushindi wakiwa na kocha Claude Puel kwa kuifunga Sparta Prague magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi ya Uropa.

Austin alifunga goli la kwanza kufuatia kutolewa penati ya utata, baada ya Costa Nhamoinesu kudaiwa kuwa ameushika mpira wakati wa kumkaba mshambuliaji huyo.

Austin tena aliongeza goli la pili kwa kichwa na kisha baadaye Jay Rodriguez akaongeza la tatu.
 Kapteni Van Dijk akiwaamua Dusan Tadic na Charlie Austin waliokuwa wakigombea kupiga penati
        Hatimaye Charlie Austin alipewa fursa ya kupiga penati na kupachika mpira wavuni
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment