Barcelona imeshindwa kupunguza pengo na vinara wa La Liga Real Madrid baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Atletico Madrid.
Baada ya kushindwa kuipenya ngome ya Atletico kwa pasi, wenyeji Barcelona walipata goli la kuongoza kupitia kwa Ivan Rakitic akiunganisha kwa kichwa krosi ya Andres Iniesta.
Katika mchezo huo Lionel Messi alilazimika kutoka nje baada ya kuumia na Atletico walitumia fursa hiyo kwa kusawazisha kupitia kwa Angel Correa.
Ivan Rakitic akiwa amepiga mpira wa kichwa uliotinga wavuni
Lionel Messi akigugumia maumivu baada ya kuumia ambapo imeelezwa atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu hivi
0 comments:
Post a Comment