LIVERPOOL YAIFUNGA ARSENAL NYUMBANI KWAO


Timu ya Liverpool imeifunga Arsenal katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza katika dimba la Emirates.

Katika mchezo huo Theo Walcott alikuwa wa kwanza kufunga goli na kuifanya Arsenal iongoze katika dakika ya 31, baada ya kukosa penati.

Philippe Coutinho aliisawazishia Liverpool kwa mpira wa adhabu alioupiga kwa umahiri, kabla ya Adam Lallana kufunga la pili baada ya mapumziko.

Coutinho alifunga goli lake la pili na Sadio Mane kufunga la nne, kabla ya Arsenal's Alex Oxlade-Chamberlain kufunga goli la jitihada binafsi na Calum Chambers kufunga la tatu kwa Arsenal.
                                                         Adam Lallana akiifungia Liverpool
                                                         Sadio Mane akiifungia Liverpool goli la nne 
                                  Simon Mignolet akipangua penati iliyopigwa na Theo Walcott
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment