HALI YA TAHARUKI YAUKUMBA UWANJA WA NDEGE WA JOHN F. KENNEDY


Abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa John F. Kennedy waliamriwa na polisi kujificha katika kitu chochote jana usiku baada ya kutolewa ripoti tata ya kutokea mlio wa risasi.

Kila abiria aliamuriwa kutoka katika lango la nane la uwanja huo, wengine kuelekezwa kwenye njia za kurukia ndege, wakati polisi wakimtafuta mtu huyo mwenye silaha ambaye hakuwepo.

Mmoja wa abiria amesema alisikia polisi akitoa amri ya kuwaambia “iwapo umesahau kuchukua kituchochote, achana nacho hakina thamani ya maisha yako, kimbia”.
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye njia ya kurukia ndege baada ya kuamuriwa na polisi kufanya hivyo
  Abiria katika uwanja wa ndege wa John. F. Kennedy wakiwa katika hali ya kutaharuki
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment