Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City wameianza ligi hiyo kwa kuduwaza na kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Hull City.
Kikosi cha kocha Mike Phelam kiliongoza kwa kufunga goli lililofungwa kwa pamoja na wachezaji Adama Diomande na Abel Hernandez hata hivyo goli hilo alipewa Diomande.
Goli hilo lilizawazishwa baadaye na Riyad Mahrez kwa njia ya penati baada ya mchezaji mpya wa Leicester City Ahmed Musa kufanyiwa madhambi.
Hull City ilipata goli la pili na la ushindi kupitia kwa Robert Snodgrass baada ya krosi aliyoipiga kushindwa kuzuiliwa na mabeki.
Goli la Hull City lililofungwa na wachezaji wawili Adama Diomande na Abel Hernandez
Riyad Mahrez akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli kwa mkwaju wa penati
Robert Snodgrass akishangilia goli la pili na la ushindi kwa Hull City alilofunga
0 comments:
Post a Comment