SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR LAPATA CRANE MPYA MBILI KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA KATIKA BANDARI ZA UNGUJA NA PEMBA


Shirika la Bandari Zanzibar lapata Crane mbili kubwa na ndogo kwa ajili ya kutowa huduma ya upakizi na ushushaji wa mizigo katika bandari yac Unguja na Pemba, kutoka kampuni ya Ujerumani iliotengeneza Crane hiyo. Crane kubwa ina uwezo wa kubeba mzigo wa tano 64 kwa wakati mmoja kushsha katika meli na kupakia katika meli kama inavyoonekana Crane hiyo ikishusha katika meli bandari ya Zanzibar.
Crane kubwa ya Shirika la Bandari ikiwa katika bandari hiyo baada ya kushushwa, Crane hiyo itapunguza tatizo la ushushaji wa mizigo katika meli wakati meli hizo zikiwa na matatizo ya crane katika meli hiyo.
Mtaalamu wa Kampuni ya Ujerumani iliotengeneza Crane hiyo akitumia remote ya kuongozea Crane hiyo wakati ikiwa katika bandari ya Zanzibar.
Crane Ndogo ya Shirika la Bandari ikishushwa katika Meli hiyo ambayo itatumika katika Bandari ya Mkoani kisiwanin Pemba. Kwa hisani ya ZanziNews
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment