Raia wa Tunisia ambaye aliendesha lori na kugonga kundi la watu Jijini Nice, Ufaransa alifanya utafiti siku kadhaa kabla ya kufanya shambulizi hilo.
Ripoti zinasema Mohamed Lahouaiej-Bouhlel aliendesha kwenye barabara ya kando ya ufukwe wa bahari wa Promenade siku ya jumanne na jumatano kama maandalizi.
Zaidi ya watu 80 walikufa kwa kugongwa na lori alilokuwa akiliendesha wakati wakiwa katika eneo hilo la ufukwe wakisherehekea sikukuu ya Bastille kwa kuangali fataki, Alhamisi.
0 comments:
Post a Comment