Bondia Deontay Wilder anataka kuzichapa na Tyson Fury na Anthony Joshua baada ya kufanikiwa kutetea mkanda wake wa uzito wa juu wa WBC, kwa ushindi wa KO dhidi ya Chris Arreola.
Mmarekani huyo mwenye miaka 30, alimdhibiti Arreola, kwa kumbana vilivyo kwa makonde kwenye kona katika raundi ya nane na mchezo huo kukoma katika raundi hiyo huko Birmingham, Alabama.
Ushindi huo wa Wilder ameupata licha ya kuhisiwa kuvunjika mkono wake pamoja na kuchana misuli ya kwenye mikono wakati wa pambano hilo.
Ngumi nzito ya kushoto ya Deontay Wilder ikimuingia vilivyo Chris Arreola
Deontay Wilder akimpiga konde Chris Arreola licha ya kwenda chini
0 comments:
Post a Comment