DONALD TRUMP AWAAHIDI WAMAREKANI KUTOKOMEZA VITISHO VYA USALAMA


Donald Trump ameahidi akiwa rais atakabiliana na matukio ya vitisho vinavyoikabili Marekani, katika hotuba yake ya kukubali kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican.

Katika hotuba yake hiyo hiyo kwenye mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho huko Cleveland, Bw. Trump ameahidi kuwa ghasia ambazo kwa sasa zinaliathiri taifa la Marekani, zitamalizika mapema.

Akiainisha namna serikali yake itakavyoendeshwa Trump, amesema dola yake itafungua mustakabali mpya kwa Wamarekani, kwa kuweka maslahi ya Marekani kwanza pamoja na wananchi wake wa kawaida.
Donald Trump akiwa na mtoto wake mdogo wa kiume Barron, mkewe Melania kushoto, pamoja na mgombea mwenza wake Mike Pence na mkewe Karen, baada ya kumaliza hotuba yake.

You might also like:
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment