WATU WANNE WAUWAWA KWA RISASI JIJINI TEL AVIV NCHINI ISRAELI

Wapalestina wawili wenye bunduki wameuwa watu wanne na kujeruhi sita baada ya kufyatua risasi kwenye eneo la wazi la manunuzi na hoteli kati kati ya Jijini Tel Aviv, Mamlaka za Israeli zimesema.

Mashambulizi hayo yamefanyika kwenye maeneo mawili tofauti katika Soko la Sarona, lililopo karibu na Wizara ya Ulinzi ya Israel na Makao Makuu ya jeshi.

Polisi wamesema watu hao wawili wenye silaha wanatokea Yatta, katika kijiji cha Palestina kilichopo karibu na mji wa Hebron huko West Bank.
Polisi wa Israeli wakimdhibiti mtu mmoja na kumvua nguo baada ya kumshuku kuwa huenda alikuwa amevaa milipuko
          Madaktari wakihaha kujaribu kuokoa maisha ya mtu mmoja aliyejeruhiwa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment