Ni miezi miwili tangu nchi ya Japan ikumbwe na matetemeko mawili ya ardhi yaliyopelekea zaidi ya watu 50 kupoteza maisha na maelfu kujeruhiwa katika mji waKumamoto nchini humo. Tangu matetemeko hayo yatokee ni zaidi ya watu 200 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa tetemeko la ardhi.
Wagonjwa hao hupata kizunguzungu, kichefuchefu na kukosa nguvu, pia inasemekana bado wanapata hisia za hofu na wasiwasi juu ya maisha yao na wakihisi kuna uwezekano tetemeko lingine linaweza kutokea na kuhatarisha maisha yao. Hali hii wameiita ‘jishin-yoi’ ikiwa ina maanisha ‘ulevi wa tetemeko la ardhi’.
Matetemeko hayo mawili yalipelekea zaidi ya nyumba 410,000 kubaki bila maji na nyingine 200,000 bila umeme hali iliyosababisha watu wengi kukaa katika foleni kwa ajili ya chakula na maji katika vituo vya misaada ya dharura, Japan imekua ikikumbwa na matukio ya namna hii mara kwa mara.VIDEO TETEMEKO HILO LILIVYOSABABISHA MAAFA JAPAN>>
0 comments:
Post a Comment