PICHA: Yanga wamekamilisha usajili wa staa wa kimataifa


Usiku wa June 17 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilitangaza good news kwa mashabiki wake, baada ya zile tetesi ambazo zilikuwa zimeenea mchana wa siku hiyo, kuthibitika kuwa ni kweli.
Sasa ni rasmi Yanga imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia aliyekuwa anaichezea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe Obrey Chirwa kwa mkataba wa miaka miwili. Ada ya uhamisho Yanga wenyewe hawajaweka wazi ila soccer24.com walitanga staa huyo kusajili kwa dola 100000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 za kitanzania.
Page-36-Obrey-Chirwa-FC-Platinum-striker-left-sunk-the-Dembare-ship-at-Mandava-fortress-with-a-brace-last-Saturday.
Orey Chirwa ambaye yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini umri wa miaka 23, anakuwa staa wa tatu kujiunga na Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, baada ya Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kusajili na wao wakitokea klabu hiyo msimu uliopita.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment