Ora alianza December mwaka jana kwa kuishtaki label ya Roc Nation na baadaye label hiyo nayo kumshtaki kwa madai kuwa hakukamilisha makubaliano ya mkataba wao.
Gazeti la Mirror limeripoti kuwa makubaliano mapya yamefikiwa ya kumaliza suala lao nje ya mahakama. Ora pia alitumia mtandao wa Snapchat kueleza habari njema kuwa anasaini mkataba mpya.
Mirror imeripoti kuwa msanii huyo amesainishwa na Warner Music.
Ora alisaini mkataba wa kurekodi album tano na Roc Nation mwaka 2008 akiwa na miaka 18. Hata hivyo amefanikiwa kutoa album moja tu, ORA ya mwaka 2012.
Alidai kuwa baada ya Roc Nation kuanza kujihusisha na uwakala wa michezo aliachwa solemba. Alishtaki kutaka atoke kwenye label.
Jay Z naye alimshtaki akitaka walipwe dola milioni 2.4 kwa madai kuwa walitumia dola milioni 2 kwenye masoko na promotion kwaajili ya album ya pili ya Ora ambayo hata hivyo bado haijatoka.
0 comments:
Post a Comment