MASHABIKI WA CROATIA WARUSHA FATAKI UWANJANI NA KUIBUA TAHARUKI


Fataki imelipuka mbele ya wasimamizi wa uwanja wakati mashabiki wa Croatia walipoanza kurusha fataki hizo uwanjani na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe katika mchezo ulioishia kwa sare ya magoli 2-2 dhidi ya Jamhuri ya Czech.

Kufuatia kitendo hicho EUFA itakaa kikao cha nidhamu hii leo baada ya kupata ripoti ya refa Mark Clatternburg kuhusina na tukio hilo, wachezaji wa Croatia wanahofia kuwa timu yao huenda ikaondolewa kwenye michuano hiyo.

Croatia walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-1 wakati urushaji fataki hizo uwanjani uliofanywa kwa kupangwa na mashabiki ulipoanza, wachezaji walijaribu kuwasihi wasifanye hivyo lakini mashabiki wao hawakusikia na badala yake waliwarushia vitu.
Wachezaji wa Croatia wakijaribu kuwasihi bila ya mafanikio mashabiki wao kuacha kurusha fataki uwanjani
Mmoja wa wasimamizi wa uwanja akielekea kuanguka chini baada ya fataki kulipuka karibu yake
                Mashabiki wa Croatia wakidundana ngumi uwanjani wakati wa ghasia hizo
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment