Mabingwa mara mbili wa kombe la Euro timu ya Hispania wamesonga mbele hatua ya 16 bora, kwa kusakata kabumbu safi dhidi ya wachovu Uturuki katika mchezo ulioishia kwa ushindi wa magoli 3-0, huko Nice, Ufaransa.
Kwa rekodi za michuano hiyo ya Euro 2016, Hispania imekuwa timu ya kwanza kufunga magoli zaidi ya mara mbili. Katika mchezo huo Alvaro Morata aliipatia Hispania goli la kwanza na Nalito kuongeza la pili kisha Morata kumalizia la tatu.
Cesc Fabregas akidhibitiwa vilivyo na wachezaji wa Uturuki
Nalito akiwa ameupachika mpira wavuni na kumpoteza maboya kipa wa Uturuki
0 comments:
Post a Comment