GWIJI LA SOKA PELE AMUAMBIA MARCUS RASHFORD ASIOGOPE

Gwiji la Soka Pele amempatia ushauri mmoja tu mchezaji kinda, Marcus Rashford, anayeelekea kucheza michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa, kwa kumumbia neno moja tu 'Usiogope'.

Mkongwe huyo wa Brazil Pele aliitwa kuchezea timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 16 na alishinda kombe lake la kwanza la Dunia mwaka moja baadaye 1958.

Rashford, 18, alikuwa anachezea timu ya taifa chini ya miaka 21 mwaka moja uliopita, lakini sasa amepanda na anachezea timu ya wakubwa ya taifa ya Uingereza chini ya kocha Roy Hodgson.
Marcus Rashford akiwa mazoezini na timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama Simba Watatu.

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment