CROATIA YAIDUWAZA HISPANIA NA KUISUKUMIA MDOMONI MWA ITALIA 16 BORA


Timu ya Hispania itakutana na Italia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016, inayoendelea nchini Ufaransa baada ya Croatia kuwafunga magoli 2-1 katika mchezo wa jana usiku wa kundi D.

Katika mchezo huo Hispania iliongoza baada ya Cesc Fabregas kunyanyua mpira juu ya kipa Danijel Subasic na kisha Alvaro Morata kuudokoa na kuutumbukiza wavuni.

Croatia iliandika goli la kusawazisha kupitia kwa Nikola Kalanic akiunganisha krosi ya Ivan Perisic. Kipa Subasic aliokoa penati iliyopigwa na Sergio Ramos. Goli la dakika za mwisho la Perisic liliwapa Croatia ushindi.
                                   Nikola Kalanic akimpoteza mahesabu kipa David De Gea
Kipa David De Gea akibaki analalamika baada ya kufanya uzembe na kujikuta akiruhusu goli la pili lililofungwa na Ivan Perisic
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment