Mei 6 2016 Waziri wa Viwanda, biashara na Uwekezaji Charles Mwijage aliwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Katika hotuba yake, Waziri Mwijage aligusia sekta mbalimbali kama vile Viwanda vidogo na Biashara ndogo, Masoko. ..>>>’Ujenzi wa uchumi wa viwanda ni vita, tena vita kubwa sana. Mafanikio katika uchumi wa viwanda yatasababisha nchi yetu kuwa Taifa la watu wa kipato cha kati‘
‘Katika mwaka 2016/2017, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya Shilingi Milioni 20 ikilinganishwa na lengo la Shilingi Milioni 12 na elfu 14 kwa mwaka 2015/2016 kutokana na ada za leseni, uuzaji wa nyaraka za zabuni, faini kwa kukiuka Sheria ya leseni na makusanyo mengineyo‘
‘Katika mwaka 2016/2017, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaomba kutengewa jumla ya Shilingi 81,871,992,000, ili kutekeleza majukumu ya Wizara. Ni jukumu kubwa na nyeti ambalo linapaswa kuendelea kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote hasa Watanzania wazalendo‘
Unaweza kuendelea Kumsikiliza hapa chini kwenye hii video….
0 comments:
Post a Comment