The Industry Yatambulisha Rasmi Wasanii Wake Mbele ya Waandishi wa Habari leo


THE INDUSTRY MUSIC LABEL

TAARIFA KWA UMMA

THE INDUSTRY YATAMBULISHA RASMI WASANII WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI
Kampuni ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Producer wa Music Nahreel siku ya leo tarehe 6 mwezi wa Tano 2016 imewatambulisha wanamuziki wake watatu wapya ambao watakuwa chini ya usimamizi wa label hiyo.

Kati ya wasanii hao watatu wawili ni wake kike ambao ni Rosa Ree na Seline na Wakiume mmoja ajulikanae kwa jina la Wildad

The Industry wamesema kazi zao zitaanza kuchezwa redioni na kwenye TV siku si nyingi  ambapo jumatatu ijayo wataachia wimbo wa Seline pamoja na Video yake

The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.
Imetolewa na,
The Industry PR
Nahreel Akiongea na Waandishi wa Habari , Kulia kwake ni Seline , Kushoto ni Rose Ree na Aika

Kutoka Kulia ni Wildad , Aika na Rose ree Wakisikiliza kwa Makini Maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari leo

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment