Ni wengi ambao hawakuwa na mawazo wala kuamini kuwa msimu huu klabu yaLeicester City itachukua Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya kwanza toka ianzishwe miaka 132 iliyopita, lakini wengi hawakuishia kutokuamini kwa mdomo wengine waliweka ahadi za kutekelezeka.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza na timu ya taifa ya Misri Ahmed Hossam ‘Mido’ ambaye sasa hivi ni mchambuzi wa masuala ya soka beIN Sports alikuwa ni moja kati ya watu wasiotarajia kuona hilo linatokea na kuhaidi kuwa kama Leicester watatwaa taji la EPL atanyoa nywele zake ambazo zimekuwa kama ndio utambulisho wake.
Mido amelazimika kutekeleza ahadi yake aliyoiweka kwa kunyoa kama alivyohaidi mapema mwezi January,, Kabla ya kustaafu Mido amewahi kuzichezea Ajax, Marseille,Roma, Middlesbrough na West Ham. Lakini Mtangazaji wa BBC Garry Lineker alihaidi na yeye kama Leicester watatwaa EPL atafanya kipindi chake cha TV na nguo ya ndani.
Video wakati akihaidi kuhusu kunyoa nywele
0 comments:
Post a Comment