Baada ya jezi za msimu ujao wa 2016/2017 kwa baadhi ya timu kuonekana zikivuja katika mtandao wa 101greatgoals.com leo May 4 2016 klabu ya Chelsea ya Uingereza imeonesha rasmi jezi zake itakazotumia msimu wa 2016/2016 katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu Uingereza.
Jezi mpya za Chelsea ambazo zimeoneshwa leo May 4 2016 zitapatika kwa gharama ya pound 90 ambazo ni zaidi ya Tsh laki mbili na elfu hamsini bila kuprintiwa namba na jina, jezi mpya za Chelsea watazivaa kwa mara ya kwanza katika mechi yao ya mwisho ya msimu wa 2015/2016 dhidi ya mabingwa wapya wa EPL Leicester City.
Chelsea bado wanaendelea kuvaa jezi zilizotengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani Adidas, lakini bado kifuani zinaendelea kuwa na nembo ya kampuni ya matairi ya Yokohama ambao wana mkataba na kampuni hiyo wenye thamani ya pound milioni 200.
0 comments:
Post a Comment