Mshambualija hatari Cristiano Ronaldo ameifungia Real Madrid magoli mawili na kuisaidia kuifunga Deportivo La Coruna, magoli 2-0 hata hivyo hayakuisaidia kuizuia Barcelona kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania.
Mshambuliaji huyo Mreno aliyeonekana akiwa katika ubora wake hapo jana alipachika magoli hayo mawili katika dakika 25 za mwanzo za mchezo huo, na mara mbili aligonga mwamba wa goli kabla ya mapumziko.
Hata hivyo Real Madrid walishinda mchezo wao wa mwisho wa La Liga, walijikuta wakimaliza pointi moja nyuma ya Barcelona ambayo ilimfunga Granada mabao 3-0, magoli yote yakifungwa na Luis Suarez.
Kwa matokeo hayo Barcelona imetwaa, ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania na huenda wakatwa mataji mawili kwa mara ya pili mfululizo pale itakapofanikiwa kuifunga Sevilla katika kuwania kombe la Copa del Rey katika mchezo wa fainali Mei 22.
Cristiano Ronaldo akimpoteza mahesabu kipa wa Deportivo La Coruna na kupachika goli.
Karim Benzema akikatiza kati kati ya mabeki wa Deportivo La Coruna
Luis Suarez akiruka juu kufurahi moja ya magoli aliyoyafunga jana
Luis Suarez akimtabaza kipa wa Nantes na kupachia goli
0 comments:
Post a Comment