Kabla ya kudundwa kwenye raundi sita, Khan alitumia vyema kasi yake nzuri na kutamba ulingoni vyema jambo lililokuwa likimsumbua mpinzani wake na alionekana akiongoza vizuri kwa pointi.
Hata hivyo pale Khan alipopoteza umakini kwa sekunde chache tu, bingwa wa mkanda huo Saul 'Canelo' Alvarez alimpiga ngumi nzito ya kulia iliyomlaza chini Khan na kushindwa kunyanyuka kupambana tena.
Canelo akimpiga Amir Khan ngumi ya kulia iliyompeleka chini
Amir Khan akiwa chali ulingoni baada ya kupigwa ngumi nzito na Canelo
Refa wa pambano hilo akimaliza mchezo baada ya Khan kuwa hoi
0 comments:
Post a Comment