BAYERN MUNICH WASHEREHEKEA UBINGWA KWA KUMWAGIANA BIA


Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola, alijikuta kitota kwa kumwagiwa bia wakati akisherehekea na wachezaji wake ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Hannover.

Kocha huyo ambaye anajiunga na Manchester City msimu ujao, timu yake ilishakuwa imelitwaa taji hilo hata kabla ya mchezo huo wa jana, ambao Robert Lewandowski alikuwa wa kwanza kuifungia Bayern goli la kwanza na kuweka rekodi ya kufunga magoli 30 katika msimu huu.

Kiungo wa Ujerumani, Mario Gotze, aliongeza la pili kwa jitihada binafsi nzuri, na kisha kuongeza la tatu katika kipindi cha pili kabla ya Artur Sobiech hajaifungia Hannover goli pekee katika mchezo huo.
     Cheers ya ubingwa kocha Pep Guardiola akigongesha glasi na mchezaji wake
             Wachezaji wa Bayern Munich wakimwagia bia kocha wao Pep Guardiola
     Kocha Pep Guardiola akimwagia bia mmoja wa watumishi wa Beyern Munich
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment