Baada ya kutwaa Laliga, FC Barcelona wametwaa Kombe la pili leo May 23 2016


Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Hispania kwa klabu ya FC Barcelona ya Hispaniakufanikiwa kuibuka na Mabingwa, usiku wa May 22 2016 walifanikiwa kutwaa taji la pili baada ya kufanikiwa kuifunga Sevilla katika mchezo wa fainali ya Kombe la Copa del Rey.

Fainali hiyo ambayo ilikuwa inakutanisha Mabingwa wa Europa League Sevilla na Mabingwa wa Ligi Kuu Hispania klabu ya FC Barcelona ilimalizika kwa FC Barcelonakuibuka na ushindi wa goli 2-0, hadi dakika 90 zinamalizika kulikuwa hakuna timu iliyofanikiwa kuona nyavu za mwenzake, hivyo muamuzi akalazimika kuongeza dakika 30.
Dakika 30 za nyongeza ndio zilikuwa mbaya zaidi kwa klabu ya Sevilla, kwani dakika ya 7 baada ya kuanza kwa dakika 30 za nyongeza, Jordi Alba alipachika goli la kwanza na kuifanya FC Barcelona iendelee kutawala mchezo, sekunde kadhaa kabla ya dakika 120 kukamilika Neymar alifanikiwa kupachika goli la pili.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment