Uganda yathibitisha kupitishia bomba lake la mafuta Tanzania na siyo Kenya

Nchi ya Uganda imefikia maamuzi ya kuamua kujenga bomba lao la mafuta lipitie nchini Tanzania na siyo Kenya.140905102638_kenya_oil_640x360_bbc_nocreditHivi karibuni rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alifanya ziara nchini Ufaransa kwenye kampuni ya Total ili kufanya uwezekano wa bomba hilo lipitie nchini kwake.
Mwanzoni nchi ya Uganda ilikuwa imezungumzia nia ya kujenga bomba la mafuta yake kupitia Kenya lakini baada ya mkutano na rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli, rais wa Uganda Yoweri Museveni wameibwaga Kenya.
Bomba h
ilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga ambapo mwanzo nchi ya Kenya walitaka lipitie kwenye bandari ya Lamu.
Makampuni matatu ya uchimbaji mafuta ikiwemo Total ya Ufaransa, CNOOC ya China na Tullow ya Uingereza ndiyo zinazomiliki leseni ya kuchimba na kusafisha mafuta nchini Uganda.
Aidha nchi ya Uganda imefikia uamuzi huo kutokana na kuwa na wasiwasi na kundi la Alshabab kushambulia bomba lake endapo watalipitishia nchini Kenya.
Ujenzi huo utakapoanza unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 15,000 kwa vijana wasiokuwa na ajira.
140905102638_kenya_oil_640x360_bbc_nocredit
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment