Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, afisa masoko wa Steps Entertainment, Kambarage alisema filamu hiyo ya Dotto inazungumzia matatizo mbalimbali ambayo yanatokea kwenye familia na kusababisha mpasuko.
“Kwenye familia nyingi ambazo ni changa mara nyingi kuna ugomvi unatokea baina ya wazazi na watoto, kwa hiyo haya yote yataonekana kwenye filamu, ni filamu nzuri sana. Irene Paul amevaa uhusika kweli kweli,” alisema Kambarage.
Pia Kambarage alisema katika uzinguzi huo hakutakuwa na kiingilio, na nikuanzia saa 2 usiku.
0 comments:
Post a Comment