MAZOEZI YA KIKOSI MAALUM CHA ULINZI SAUDI ARABIA NI BALAA

Picha za mazoezi ya kikosi maalum cha wanajeshi wa Saudi Arabia zenye kuonyesha uwezo na ujuzi wa hali ya juu, mithili ya filamu za kuigiza, lakini hizi ni za kweli na si maigizo zimekuwa kivutio mno.

Kikosi hicho cha wanajeshi wakakamavu wa Saudi kimeonekana kikifanya mazoezi ya kuonyesha uwezo wao wakati wa mazoezi ya kijeshi jangwani mashariki mwa mji wa Riyadh, Saudi Arabia.

Katika moja ya picha za kustaajabisha inaonyesha wanajeshi wawili wa Saudi Arabia wakiwa wanaruka juu ya magari mawili ya polisi yanayotembea wakiwa na silaha mikononi huku wakifunika nyuso zao na kitambaa cheusi.
 Wanajeshi wa Saudi Arabia wakiwa wamepaa juu ya magari yanayotembea huku wenzao wawili wakiwa nchini wakati wa mazoezi yao
                            Mazoezi hayo pia yalihusisha milipuko kama inavyoonekana
    Kipande cha tofali kikivunjwa kwenye kichwa cha mmoja wa wanajeshi wa Saudi Arabia
You might also like:
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment