Tottenham imeendelea kujiimarisha katika kutoa changamoto ya kuwania kutwaa kombe la Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuichakaza Manchester United kwa mabao 3-0.
Baada ya kushuhudia Leicester ikiishinda Sunderland katika mchezo wa mapema jana, Tottenham ilifunga magoli yote matatu katika kipindi cha pili.
Dele Alli alipachika la kwanza na kisha Toby Alderweireld kupiga la pili kwa kichwa, kabla ya Erik Lamela kumalizi la tatu.
Dele Alli akifunga goli la kwanza kwa Tottenham
Anthony Martial akijaribu kuwatoka mabeki wa Tottenham
Katika mchezo mwingine jana Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Stoke City, huku Mbelgiji Divock Origi mwenye asili ya Kenya akipachika mabao mawili.
0 comments:
Post a Comment