MADEE ASEMA MAREHEM PENDO NDIYE ANAYEMFANYA ASIMTUPE DOGO JANJA


Yawezekana wewe ni mmoja kati ya Watu wanaojiuliza Madee anatoa wapi Spirit ya Kumsukuma Sana Dogo Janja Kiasi kwamba amemfanya kama Mwanaye wa Kumzaa kwa Kumpa Kila anachostahiki kukipata Mtoto wa Kifahari.
Utakuwa na kumbukumbu kwamba Dogo Janja alikuwa Chini ya Vijana wa Jambo Squad kabla ya Kuonana na Kuchukuliwa na Madee, Baadae Dogo Janja alimkosea Madee na Madee Kuamua Kumtema. Janjaro akaja Akachukuliwa na Kampuni ya Mtanashati Entertainment inayomilikiwa na Ostaz Juma Namusoma na Akiwa Chini ya Ostaz Juma Janjaro alimsema Mengi Madee ila Ndoa yake pia Mtanashati nayo Ikavunjika.
Janjaro akarudi Nyumbani tena na Kuwa na Jambo Squad na Baadae tena Madee akamchukua Bila kujali Mengi Mabaya aliyotendewa na Dogo Janja.
Juzi kati Madee akamnunulia Gari ya Pili Dogo Janja tena Kimsingi Utajijibu kuwa Lazma Kuwe Kuna Sababu ya Msingi inayomfanya Madee Aamue kufanya yote haya.
Sasa Nimepiga Stroy na Madee Kupitia Kipindi cha FUNIKO BASE cha Radio5 na Madee amefunguka kwa kusema anampenda sana Dogo Janja ukianchana na mambo yao ya kimuziki sababu kipindi Fulani alikuwa na girlfriend wake marehemu Pendo kuna kitu ambacho Pendo amewahi kuongea kwenye maisha yake kuwa akimaliza shule akiwa na hela atatamani kuishi na mtoto ambaye siyo mtoto wake na atamlea kama mtoto wake , sauti hiyo imekuwa Ikimrudia Madee Mara kwa Mara  kwenye kichwa chake tangu alivo fariki tuu kitu ambacho kinazunguka kwenye ubongo wake ni kauli  hiyo kila siku anapowaza kauli hiyo anamkumbatia Dogo Janja na ukimuuliza ana Watoto wangapi atakwambi  ana watoto wawili mmoja anaitwa SAIDA na Mwingine ABDULI.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment