Barcelona yavuliwa ubingwa barani ulaya Uefa




Katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya timu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti.
article-3538592-3329EFBA00000578-170_964x395
Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.
Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .

33267B1500000578-0-image-a-44_1460582929366
Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .
Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment