WAPIGANAJI WA KIKURDI WAKIRI KUHUSIKA NA MILIPUKO YA UTURUKI

Kundi la wapiganaji wa Kikurdi la TAK limesema ndilo lililofanya shambulizi baya kubwa katika Jiji Kuu la Ankara nchini Uturuki.

Taarifa iliyotolewa kwa njia ya mtandao kundi hilo limesema shambulio hilo lililouwa watu 37 ni la kulipa kisasi dhidi ya operesheni za kijeshi eneo la Wakurdi la kusini mashariki.

Wapiganaji wa kundi la TAK, ambao ni sehemu ya Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) kilichopigwa marufuku, wamesema ndio pia waliohusika na mlipuko wa bomu la Ankara mwezi uliopita.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment