Waongozaji Video wa nje Wanavyozidi Kuingiza Pesa Kutoka Bongo..Wakina Adamu Juma Wanakosea Nini?

Muziki wa Tanzania kwa sasa umefanikiwa kuchukua nafasi kubwa Afrika na tayari umeanza kupenya kwenye nchi nyingine duniani.

Wasanii wengi wenye menejimenti nzuri yenye uwezo wa kifedha wanaonekana kukimbilia nchi za jirani kufanya video na madirector wa huko, pamoja na kuzitumia location za huko kwenye video zao.

Madirector wa bongo kwa sasa wanaonekana kuzikosa fedha nyingi za wasanii. Alianza AY na Jaydee kwenye safari hizo za nje kabla ya Diamond kuunga msafara huo na wengine kufanya msururu huo kuwa mkubwa.

Mafanikio ya kwenda huko yameonekana, rangi za video zimekuwa nzuri na baadhi ya video zimeshaanza kupigwa kwenye TV kubwa za nje na kutengeneza connection kubwa. Zipo video zinazopigwa kwenye TV hizo za nje lakini zimetengezezwa na madirector wa ndani kama Hanscana, GQ na wengine.

Godfather na Justine Compus ndiyo madirector wanaoongoza kuchukua fedha za wasanii wa bongo kama; Diamond, Navy Kenzo, Joh Makini, Vanessa Mdee, Jux, Shettah na wengine wengi. Hatua hiyo imepelekea mpaka wasanii wanaochipukia kutamani kufanya kazi na madirector hao wa nje kama Kleyah alivyofanya kwenye ‘African Drum’.

Adam Juma amekosa nini wakati ameweza kufanya video kibao nzuri ambazo zimewafikisha wasanii wengine leo hapa walipo, ukiingalia video ya ‘Mawazo’ ya Diamond ilikuwa ni nzuri kwa kipindi kile. Je Adam Juma alikosea wapi ambapo Nisher alitakiwa kuparekebisha?

Kwanini hizo milioni thelathini za kutengeneza video wasipewe madirector wa ndani ili watafute vifaa vilivyo vizuri ili watengeneze video zenye viwango kama kweli hilo ndiyo tatizo. Kwanini afatwe Godfather Afrika Kusini wakati D’ Banj na Don Jazzy bado hawafikirii kuja Tanzania kufanya video na Khalfani Almando?
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment