Kikosi
kazi maalumu cha kuchunguza makosa ya kihalifu kimekamilisha uchunguzi
wa tuhuma za usafirishaji Tumbili 61 zinazowakabili raia wawili wa
Uholanzi na Watanzania wawili.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alilithibitishia
gazeti hili jana kukamilika kwa uchunguzi huo na kusema jalada
limepelekwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
Kauli
ya Mutafungwa imekuja wakati kuna uvumi uliozagaa kuwa watuhumiwa hao
wataachiwa huru wakati wowote kuanzia jana bila kufunguliwa mashtaka.
Kamanda
Mutafungwa alisema kuwa wao kama chombo cha uchunguzi, wametimiza
wajibu wao na mwenye uamuzi wa kushtaki au kutoshtaki ni Mkurugenzi wa
Mashtaka Nchini (DPP) baada ya kupitia ushahidi.
Hata
hivyo, alisema kuwa watuhumiwa hao wanne bado wanashikiliwa na polisi
wakisubiri maelekezo ya kisheria ya DPP, hivyo siyo sahihi watu
kuvumisha kuwa wameachiwa bila masharti.
Watuhumiwa
hao ni Mkurugenzi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles
Mulokozi na Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, Utalii wa
Picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika. Watuhumiwa wengine ni
raia hao wa Uholanzi ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik
Vardanyian (52) na Eduard Alik Vardanyian (44).
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alipoulizwa juzi
kuhusu uvumi wa kutoshtakiwa kwa watuhumiwa, alisema yeye ametimiza
wajibu wake.
0 comments:
Post a Comment