Rais Magufuli
ametoa zawadi ya vyakula na vinywaji vyeye jumla ya Shilingi milioni
tisa na laki tatu katika vituo vya malezi kwa Wazee na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu nchini ili kusherekea sikukuu ya pasaka.
Akitoa zawadi hizo kwa niaba ya Rais Magufuli Naibu kamishna wa Ustawi wa jamii Rabikira Mushi alisema..‘Awali
ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru mwenyez Mungu kwa
kutujaalia sote kujumuik mahali hapa kwa ajili ya tukio hili muhimu la
kukabidhi zawadi za sikukuu kutoka kwa Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli‘ >>> Rabikira Mushi
‘Aidha
shukrani hizi napenda pia zimfikie mheshimiwa Rais kwa upendo wake wa
dhati kabisa na kuona umuhimu wa kushiriki kutoka kusherekea sikukuu ya
Pasaka kwa pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto
walio katika mazingira hataridhi na wazee wanaolelewa katika vituo‘ – Rabikira Mushi
0 comments:
Post a Comment