Kila
tarehe 24 March dunia huadhimisha siku ya ugonjwa wa kifua kikuu, Siku
hii ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kuendeleza
mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.
Leo March
24 2016 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu alikutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuelezea
kuhusu changamoto za ugonjwa huo.
‘Kifua
kikuu ni ugonjwa unaoambukizwa na bakteria wanaojulikana kwa jina la
Mycobacteria tuberculosis, vimelea vyake huenea kwa njia ya hewa na
havichagui aina ya mtu pia hutoka kwa mgonjwa ambaye hajaanza matibabu
na kuambukiza wengine‘ ;-Ummy Mwalimu
‘Licha
ya kuwa kifua kikuu kinatibika, lakini ndio ugonjwa pekee wa kuambukiza
unaosababisha vifo vya watu wengi katika jamii, ambapo watu watatu
hufariki kila baada ya dakika moja. Takwimu zinaonyesha Tanzania
takribani watu 12,000 hufariki kwa ugonjwa huu‘ ;-Ummy Mwalimu
‘Natoa
wito kwa wananchi wote kuwa na kawaida ya kufanya uchunguzi wa afya zao
ili kugundua tatizo mapema na kuzuia kuenea kwa Kifua kikuu, tukifanya
hivyo tutapunguza kuenea kwa ugonjwa huu‘ ;-Ummy Mwalimu
0 comments:
Post a Comment