Jana 31/03/2016, Mkuu wa wilaya Iringa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa
ameshiriki kwenye mazishi ya Mnywarwanda Jeannnete Mukashema
aliyefariki kwenye ajali iliyotokea usiku Juzi. Bi Jeanette alikuwa
akisafiri na mtoto wake ( pichani juu akiwa na mkuu wa wilaya ) ambaye naye aliumia kwenye ajali hiyo na bado
anaendelea na matibabu.
Akizungumza
katika mazishi hayo, Mh Kasesela alisema, " Imeniuma sana kwani
niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo
tolewa juu kwenye basi, ni wazi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na
nguo zangu zikiwa na madoa ya damu , tulimpokea akiwa tayari amefariki.
Mkuu
huyo wa wilaya ya Iringa aliendelea kusema kuwa, " Kesho yake mtoto
alipozinduka akaanza kumtafuta mama yake, nilipomtembelea asubuhi,
nilijua mama yake amefariki dunia nilishindwa kumwambia leo alipo niona
ameanza kulia amenikumbusha nikiwa miaka 11 nilipo ondokewa na mama
yangu. lakini naamini yuko katika mikono salama, Mungu ni mwema baba
yake na ndugu wengine wamekuja kutoka Rwanda, alisema Kasesela.
0 comments:
Post a Comment