Gareth Bale amekuwa mchezaji kutoka Uingereza kufunga magoli mengi katika ligi ya Hispania ya La Liga wakati Real Madrid ikiichakaza Sevilla katika mchezo uliopigwa jana kwenye dimba la Bernabeu.
Mchezaji huyo wa Wales aligonga mwamba mara mbili, kabla ya kufunga goli lake la 43 akiwa ligi ya Hispania na kumshinda Muingereza Gary Lineker ambaye alikuwa akishikilia rekodi hiyo.
Madrid iliongoza kupitia kwa Karim Benzema kwa goli kali, huku Kevin Gameiro wa Sevilla akikosa penati na Cristiano Ronaldo na Jese, nao wakipachika mabao katika mchezo huo ambao Reala walioibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Karim Benzema akipiga shuti lililojaa wavuni
Gareth Bale akiwa juu angani akifanya vitu vyake dimbani
Matokeo mengine ya ligi Hiyo ni Villarreal 2-2 Barcelona, Valencia 0-2 Celta de Vigo na Espanyol 2-1 Ath Bilbao.
0 comments:
Post a Comment